Tangazo la Uhuru wa Binadamu

Kuhusu mawasiliano ya mataifa na vikosi vya kigeni.

Sisi, watu wa dunia, tunatoa salamu kwa mataifa yote katika Jumuiya kubwa ya Ulimwengu. Tunatambua urithi wetu mbele ya Muumba wa Ulimwengu wote, unayoonekana na usiyoonekana. Tunatangaza dunia yetu hii kama sayari ya binadamu ya Mwanzo, Nyumba yetu ya kitamaduni na urithi wetu takatifu. Sasa tunaahidi kuendeleza na kuhifadhi ardhi kwa vizazi vyote vijazo. Tunatoa wito kwa  binadamu wote kutibu jamii zote kila mahali kwa hekima na haki, hapa duniani na katika Ulimwengu.

Haki za Msingi

Sisi, Watu wa Dunia, tunasharifu haja ya kuwa na uhuru kwa wote. Kwa hiyo, tunashikilia kwamba watu wote katika Ulimwengu  wameumbwa sawa na wamejaliwa na Muumba haki tukufu na zisizoondolewa. Msingi kati ya haki hizi ni kuishi kama jamii huru kwa Sayari yao ya Mwanzo, nyumba yao ya kitamaduni; haki ya kujitawala, kujitegemea, na kujieleza ubunifu; haki ya kuishi bila kukandamizwa; na haki ya kufuata  maisha ya madhumuni ya juu na wito wa juu ule Muumba ametoa kwa wote.

Mbele ya Jumuiya Kubwa ya Ulimwengu, sisi, watu wa Dunia, tunadai haki hizi za msingi kwetu na kwa Nyumba yetu ya kitamaduni, pamoja na haki ambazo zitazotokana nazo, zikiwa ni pamoja na:

 • Haki ya uhuru; Watu wa dunia watajitawala na kujitegemea, bila kuwa chini ya au kutegemea mamlaka ingine. Hakuna taifa yeyote kutoka nje ya Dunia ambayo itahalifu au kuibatilisha uhuru wa binadamu wa dunia hii.
 • Haki ya utakatifu wa dunia; Kama sayari yetu ya Mwanzo, Dunia itakuwa huru kutoka kuingiliwa au unyonyaji na mataifa ya kutoka nje ya dunia, katika mazingira ya kiakili na kimwili. Hakuna taifa yeyote kutoka nje ya Dunia itakaribia Dunia, au kukaribia uzingo wa Dunia, au kutua, au kushiriki katika biashara, ila kwa uwazi na kwa ridhaa ya Watu wa Dunia iliyopatikana kwa njia ya kidemokrasia.
 • Haki ya utakatifu wa nyenzo za kibiolojia na maumbile;. Hakuna taifa yeyote kutoka nje ya Dunia itachukua, miliki, au kuendesha nyenzo za kibiolojia au maumbile ya binadamu kwa madhumuni yoyote.
 • Haki ya kudhibiti; Kama watu asili wa sayari moja inayojulikana kuwa na maisha katika mfumo huu wa Jua na sayari zake,  tunadai mfumo huu wa Jua na sayari zake kama himaya yetu ya ushawishi. Hakuna besi ya taifa yeyote kutoka nje ya dunia inaweza kuimarishwa katika miili au vituo vinavyozunguka dunia, wala kwenye sayari nyingine au miili ya mfumo huu wa Jua na sayari zake, ila kwa idhini ya watu wa Dunia.
 • Haki ya urambazaji kwa amani; Tunadai haki ya kusafiri na kuchunguza ndani ya mfumo wetu wa Jua na sayari zake bila kuingiliwa au kuzuiawa na vikosi vya mataifa kutoka nje ya Dunia, na tunadumisha haki ya kukataa vikosi vya mataifa kutoka nje ya Dunia viingie ndani ya mfumo huu wa Jua na sayari zake.

Sisi, Watu wa Dunia, tunaona ni wajibu wetu kudai haki na kutetea haki hizi za msingi, na kutoa na kupokea misaada sambamba na haki hizo. Katika kesi ya mzozo wowote na vikosi kutoka nje ya dunia, mzigo wa kuthibitisha kutokuwa na hatia utaanguka kwa wale ambao si raia wa Dunia.

Ukadirifu

Wakati utakapokuwa ni muhimu, katika mwenendo wa mageuzi ya watu asili wa sayari, kuungana, kuvuka migogoro na tofauti ambazo zilizowatenganisha, na kuchukua kati ya nguvu za Ulimwengu mahali yake kama taifa tofauti na huru, ukifika, itabidi watangaze sababu inayowahamasisha kutekeleza mtindo huo ili uhuru huo uweze kuzingatiwa kwa heshima.

Ingawa Dunia iko na historia ndefu ya kutembelewa na mataifa mengi kutoka nje ya Dunia, hali ya sasa ni kwamba watu wa dunia wanateseka kwa sababu ya madhara ya kuingilia na mataifa kutoka nje ya Dunia. Mataifa haya ya kigeni yanatumia mkakati wa udanganyifu, ghiliba, na unyonyaji, na lengo lao ni udhibiti wa ubinadamu, kwa hivyo watasababisha upotevu wa uhuru wa binadamu na uwezo wake wa kujitawala. Sasa ni haki takatifu na wajibu wa watu wa Dunia kupinga, kukataa, na kurudisha kuingiliwa kutokana na mataifa yaliotoka nje ya Dunia, kutangaza na kulinda uhuru wetu, na uwezo wetu kujitawala kutoka kwa mataifa yote yaliyotoka nje ya Dunia.

Hebu hatia hizi zizingatiwe na wale ambao wanasimamia uhuru katika Jumuiya Kubwa ya Ulimwengu:

 • Majeshi kutoka nje ya Dunia yamekataa kufichua hadharani na kuonyesha nia asili yao na shughuli zao ndani ya na karibu na Dunia. Vikosi hivi vinafanya kazi kwa siri, sitara, na havijaalikwa au kupokewa na watu wa Dunia. Vikosi hivi kutoka nje ya Dunia havijaweka wazi utambulisho wao , ushirikiano wao wa kisiasa au kiuchumi na visasi, pamoja na mataifa ambayo vinatumikia.
 • Inazidi kuwa dhahiri kutokana na matendo yao, vikosi hivi vina nia ya kunyonya Dunia, rasilimali yake, na watu wake, na vinashiriki katika mpango wa utaratibu wa kutawala ubinadamu katika hali ya utegemezi, itakayotawalwa na mteja wa vikosi hivi vya kigeni. Vikosi hivi vya kigeni vinataka kupata biashara, nguvu ya kiuchumi, na faida ya kimkakati inayopatikana katika Dunia hii kulingana na Dunia zengine.
 • Vikosi hivi vya kigeni vimevunja sheria za kitaifa na kimataifa ya watu wa dunia, kikariri na bila adhabu. Makosa haya, ambayo bado yanaendelea mpaka leo, ni pamoja na kuruka na vyombo vyao katika anga bila ruhusa; kutekwa na usafirishaji wa binadamu bila ridhaa yao, mauaji, ubakaji, utesaji, unyanyasaji wa kijinsia, uzalishaji na binadamu, na majaribio ya kikatili, wizi na biashara ya nyenzo za binadamu na maumbile ya kibaiolojia, wizi na biashara ya rasilimali za asili za Dunia; ushawishi wa akili na  kisaikolojia kwa kutumia njia ya sitara; ukeketaji wa binadamu na wanyama; kuendesha bila ruhusa na vikwazo vya mifumo ya kijeshi ya ulinzi; na kupenya kwa siri ndani ya jamii ya kibinadamu.
 • Vikosi hivi vya kigeni vimeshauriana kwa siri mikataba na makubaliano na watu binafsi na makundi ya binadamu, bila ridhaa ya watu wa Dunia.
 • Vikosi vya kigeni vimejaribu kumshawishi na kumpoteza binadamu kwa utaratibu na kwa njia ya kupanua matumaini ya uongo na ahadi za mali, nguvu, na ulinzi; kuwaokoa kutoka janga la dunia; uanachama katika “galactic federation”, na wokovu wa kiroho na kutaalamika.
 • Vikosi hivi vya kigeni vimenyonya na kuchochea migogoro ya binadamu kwa manufaa yao. Vikosi hivi vya kigeni vimekuwa vikitia hofu binadamu kwa kutuongoza tuamini kwamba tunaweza kuishi tu kwa msaada wao na teknolojia yao ya juu, na hivyo kukuza utegemezi wetu kamili kwao na kutunyima uwezo wetu wa kuhakikisha uhai wetu.

Madai na Maazimio

Kwa hiyo, sisi, watu wa Dunia, tunatangaza kwamba mikataba yote ya awali yaliyopo au mikataba kati ya serikali yoyote ya binadamu, vikundi, ya mtu binafsi, na vikosi vya kigeni vyovyote iwe bila kuchelewa null, tupu, na daima isimamishwe. Tunadai kwamba mikataba yoyote ya makubaliano ya awali iliyopo iwekwe wazi kikamilifu. Mikataba yoyote ya mustakabali au mikataba kati ya serikali ya binadamu, vikundi, au watu binafsi na vikosi vya kigeni lazima ijadiliwe na ridhaa kamili ya Watu wa Dunia, hadharani na kwa uwazi ulioonyeshwa na mwili wa kimataifa wa kidemokrasia unayowakilisha mataifa ya watu wa Dunia.

Tunadai kwamba vikosi vyote vya kigeni sasa viwache shughuli zote na vihame na viondoke mara moja kutoka Duniani na mazingira yake ikiwa ni pamoja na Jua, Mwezi wa Dunia, na sayari yote ya mfumo huu wa Jua. Hii ni pamoja na kutoka satelaiti yoyote ya asili au bandia, pamoja na anga yote ndani ya mfumo wa Jua.

Tunadai kwamba mashirika yote ya vikosi vya kigeni ambavyo vimeimarisha au kuendesha besi Duniani, Mwezi wake, au mahali popote ndani ya mfumo huu wa Jua, vipambue besi hizi na viweke wazi maumbile yao kwa kikamilifu.

Pia tunadai kwamba binadamu wote wanaoishi ambao sasa wamo chini ya ulinzi wa vikosi hivi vya kigeni warudishwe mara moja katika afya nzuri, tena, tunadai mahesabu kamili ya binadamu wote waliochukuliwa au walio tekwa nyara na vikosi vya kigeni, pamoja na wale waliokufa katika uhamisho. Aidha, tunadai kwamba  maumbile au nyenzo za kibaiolojia za binadamu zilizochukuliwa kutoka kwa watu binafsi vihesabiwe na viharibiwe, na lengo la matumizi yao itambuliwe. Vifaa vyovyote mwilini mwa watu wanaoishi lazima vijulikane ili viweze kuondolewa kwa salama.

Tunadai taarifa kamili ya kusudi na maelezo ya mpango ya vikoso vya kigeni ya hybridization, pamoja na eneo, utambulisho, na shughuli za maisha ya suriama kati ya binadamu na vikosi vya kigeni, wawe duniani au mahali pengine.

Ijulikane katika Ulimwengu kwamba tangu wakati huu, vikosi vya kigeni vinaweza tu kuingia mfumo wetu wa Jua na sayari zake, kukaribia Dunia yetu, kuruka katika anga yetu, kukanyaga ardhi yetu, au kuingia maji yetu kwa ridhaa ya watu wa Dunia.

Sisi, kwa hiyo, tunatangaza kwamba watu wa dunia lazima wawe huru; Kwamba binadamu wote wametolewa kutoka utii wote wa vikosi vya kigeni, na kwamba uhusiano wote wa kisiasa na kiuchumi baina yao na watu wa dunia  yamefutwa kabisa; kwamba kama taifa huru katika Jumuiya Kuu ya Ulimwengu, sisi tunachukua madaraka kamili ndani ya mfumo huu wa Jua na sayari zake kuhitimisha amani, kwa ushuru wa vita, kwa usaini wa mikataba wa ushirikiano, kuanzisha biashara, na kufanya matendo mengine yote ambayo taifa iliyo huru ya Ulimwengu inaweza kwa haki na kimaadili kufanya.

Tangazo la mwisho

Basi ieleweke kwamba katika kufanya Tangazo la Uhuru wa Binadamu, sisi, watu wa Dunia, tunathibitisha mustakabali wetu na hatima yetu kama taifa ilio huru ndani ya Jumuiya Kubwa ya waangavu. Tunatambua kwamba sisi ni sehemu ya Jumuiya hii Kubwa na kwamba sisi tuna hatma ya kukutana na jamii mbalimbali kutoka nje ya dunia yetu.

Kwa wote, tunatangaza kwamba nia yetu sio ushindi au utawala katika anga. Tunatangaza kwamba haki na wajibu tunathibitisha hapa, tutathibitisha kwa jamii zote za viumbe ambavyo tunaweza kukutana navyo.

Katika kufanya Tangazo yetu ya Uhuru wa Binadamu, tunatangaza haki zetu, majukumu yetu, na marupurupu kama taifa iliyo huru ili tuweze kufuatilia umoja, amani, na ushirikiano ndani ya familia ya binadamu bila kuingiliwa zisizohitajika au zisizofai na taifa lolote au vikosi kutoka Jumuiya Kubwa. Tunatoa tangazo hili kama kielelezo cha haki yetu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na dhamira ya heshima kwa familia ya binadamu na kwa jamii zote katika ulimwengu ambazo zinataka kuwa huru.